Wajasiriamali viziwi kupitia kikundi cha MWAWAVITE wapatiwa elimu ya kodi na kuelezewa umuhimu wa kujisajili na kutambulika na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Akifungua mafunzo hayo leo tarehe 18.09.2025 katika ofisi za TRATemeke, Meneja wa TRA, mkoa wa Kikodi Temeke, Bw. Masau Malima amesema TRA inadhamiria kuwezesha mazingira mazuri ya ufanyaji biashara kwa Wajasiriamali ikiwemo kuwatambua, kuwaelimisha na kuwawezesha kufanya biashara ili kuongeza wigo wa kodi.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki hao, Bi. Flora Gohaji kwa kutafsiriwa na mkalimani wa lugha za alama, Bw. Hamis Mkana ameishukuru TRA Temeke kwa kuwaandalia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kukuza mitaji yao na kukidhi takwa la kisheria la ulipaji wa kodi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!