
Mahakama Kuu ya Masijala, Dar es Salaam, imekataa mapingamizi yaliyowekwa na Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Tundu Lissu, katika kesi ya Uhaini inayomkabili.
Lissu alikata rufaa akipinga jinsi kesi ya Ukabidhi (Committal) ilivyofanyiwa kwenye Mahakama ya Kisutu. Mapingamizi yaliyotolewa na Lissu ni pamoja na:
Uhalali wa Mahakama ya Kisutu kuendesha Committal wakati mtuhumiwa alikamatwa Mbinga, Ruvuma.
Uahirishwaji usio wa lazima wa kesi.
Uchakachuaji wa nyaraka wakati wa usikilizwaji wa Committal.
Mahakama Kuu imesema mapingamizi haya hayana msingi na kuendelea na kesi hiyo kama ilivyopangwa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!