Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jeshi la Polisi Lamuita Polepole Kutoa Ushahidi wa Tuhuma

  • 5
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi limetangaza kuwa linafanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma za makosa ya kijinai zilizotolewa na Humphrey Herson Polepole. Tuhuma hizo, kama zilivyoelezwa na mhusika kupitia mitandao ya kijamii, zinahitaji ushahidi wa kuthibitisha zitakapo wasilishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi limesema kwamba, baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, limeendelea kukusanya ushahidi na kufanya jitihada za kumpata mhusika ili aweze kutoa maelezo, ushahidi na vielelezo vitakavyothibitisha tuhuma hizo. Hii itasaidia kurahisisha hatua za kisheria kufuatia taratibu zilizowekwa na sheria za nchi.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Bwana Polepole ameelekezwa kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kutoa maelezo na ushahidi kuhusiana na tuhuma hizo. Jeshi la Polisi linasisitiza kuwa ufuatiliaji huu unafanywa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi ameongeza kuwa jitihada za kukusanya ushahidi na maelezo kutoka kwa mhusika zinaendelea, ili kuhakikisha kwamba haki inatimizwa kwa mujibu wa sheria.

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Pingamizi la Mwanasheria Mkuu Lamng’oa Mpina Uchaguzi wa Urais 2025
Next Post Mahakama Kuu Yaikataa Mapingamizi ya Lissu Katika Kesi ya Uhaini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook