Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jela Maisha Kwa Kumlawiti Mtoto Wa Miaka 4

  • 3
Scroll Down To Discover

Mahakama ya Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha imemhukumu kwenda jela kifungo cha maisha Bw. Samwel Sosteness (20) mfanyakazi za ndani, mkazi wa kata ya Nkoanekoli wilayani Arumeru baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wa chekechea mwenye umri wa miaka minne.

Akisoma hukumu hiyo Agosti 13, 2025 kesi namba 24 ya mwaka 2025 Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mhe. Itikija Nguvava alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 10, 2025 muda wa saa 7:30 mchana huko katika maeneo Nkoanekoli wilayani humo kabla ya kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 14, 2025
Next Post Kikwete, Ramaphosa na Boko Wapanga Mwelekeo Mpya wa Uwekezaji wa Maji Afrika
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook