Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUHAKIKISHA TANZANIA INAKUWA KINARA WA UCHUMI AFRIKA

  • 34
Scroll Down To Discover

Na.Sophia Kingimali.

Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali nchini ili kuhakikisha Tanzania inakuwa kinara wa uchumi barani Afrika.

Pia,itahakikisha sekta hiyo ya uchumi wa buluu unakuwa kichocheo cha uchumi wa nchi lakini uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kuhakikisha vijana wengi wanapata ajira kutokana na sekta hiyo.

Akizungumza leo Septemba 10,2025 jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano la kitaifa la uchumi wa buluu Naibu katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Abdallah Mitawi Amesema kongamano hilo linatoa dira ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano wa kupeana maarifa kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa buluu.

“Tunapojadili mustakabali wa uchumi wa buluu hatuwezi kusahau nafasi ya vijana,wanawake na sekta binafsi kwani ni wadau muhimu ambao wanapaswa kupewa kipaumbele katika sera,mafunzo na uwezeshwaji wa kifedha ili waweze kushiriki kikamilifu na kwa tija”,Amesema.

Aidha ameongeza kuwa serikali kupitia sera na mipango mbalimbali imeweka msisitizo mkubwa kwenye maendeleo ya uchumi wa buluu ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya bahari.

Amesema kuwa Tanzania imebarikiwa na rasilimali kubwa ya uchumi wa buluu ikiwemo kilomita za mraba 64 000 za bahari ya kitaifa pamoja na kilomita za mraba 223000 za ukanda wa uchumi wa kipekee(EEZ).

“Rasilimali hizi zinatumika ipasavyo na zinauwezo wa kuongeza ajira kwa vijana,kuchochea biashara na usafirishaji,kukuza utalii wa bahari na fukwe,kukuza uvuvi na usalama wa chakula pamoja na kukuza nishati jadidifu na utafiti wa kisayansi hivyo ni matumaini yangu kongamano hili limeleta wataalam mbalimbali watakaojadili kwa kina namna ya kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hii ya uchumi wa buluu”,Amesema Mitawi.

Akizungumzia changamoto, Mitawi ametaja uvuvi haramu, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa teknolojia, na uelewa mdogo wa wananchi kuwa ni changamoto zinazoathiri maendeleo ya sekta hiyo. Hata hivyo, alieleza matumaini kuwa kupitia jukwaa hilo la kitaifa, suluhisho la changamoto hizo litaweza kupatikana kwa ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na binafsi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) Prof. Tumaini Gurumo amesema kongamano hilo lina lengo la kujadili changamoto na kuona namna ya kupata utatuzi ili zisiwe kikwazo katika ukuwaji wa blue wa nchini.

Ameongeza kuwa Kauli Mbiu ya Kongamano hilo ni, Bahari yetu, Fursa yetu na Wajibu wetu, na litakuwa la siku mbili katika kujadili na kuangalia mustakabali wa namna wataweza kukuza uchumi wa Blue kwa manufaa ya taifa letu.

Kongamano hilo limeratibiwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Uchukuzi kupitia Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Zanzibar. Limejumuisha wataalamu wa mazingira, wanataaluma, wawekezaji, na wadau kutoka sekta binafsi.



Prev Post SIKU 6 KABLA YA KUKIPIGA NA YANGA…PIGO JINGINE SIMBA HILI HAPA……
Next Post KWA MAGORI, BARBARA NA MKWABI…SAPRIZI MPYA SIMBA HII HAPA…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook