
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa ufafanuzi kuhusu kushikiliwa kwa wanahabari wawili, Baraka Lucas, mwakilishi wa Jambo TV mkoani Arusha, na Ezekiel Mollel wa Manara TV.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 07, 2025 na Msemaji wa Jeshi hilo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, imeelezwa kuwa mbali na kufanya kazi katika vyombo hivyo vya habari, waandishi hao pia walikuwa wakiendesha mitandao yao binafsi ya habari mtandaoni isiyosajiliwa.
Aidha, imeelezwa kuwa mitandao hiyo ilikuwa inakiuka Kanuni ya 4(1) ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020, kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022, chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa taratibu za uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili zinaendelea na zitakapokamilika, hatua za kisheria zitachukuliwa
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!