Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Nini hufanyika abiria anapofariki ndege ikiwa angani?

  • 51
Scroll Down To Discover

Wafanyakazi wa ndege huwa na majukumu mengi. Anaweza kuanza kwa kuhudumia chakula hadi kushika maiti wakati abiria anapofariki ndege ikiwa angani.

Ikiwa abiria atafariki wakati ndege iko angani, wafanyakazi wa ndege lazima wachukue hatua za haraka.

"Kuanzia kuwahudumia abiria kama kawaida hadi kulazimika kutunza miili yao, wanapopoteza maisha. Bila kusahau kudhibiti umati," alisema Jay Robert, mmoja wa wafanyakazi wa ndege mwenye umri wa miaka 40.

"Ubongo lazima ufanye kazi mara mbili. Kwa upande mmoja, bado tunapaswa kuandaa kifungua kinywa au chakula cha jioni kwa abiria 300. Wakati huo huo, pia tunapaswa kukabiliana na kifo."

Robert ni mkuu wa kitengo cha wahudumu wa mojawapo ya mashirika makubwa ya ndege barani Ulaya. Hapo awali alifanya kazi Emirates na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 ya kufanya kazi kwenye ndege.

Kama wafanyakazi wote wa ndege, Robert ana mafunzo ya kukabiliana na vifo vya abiria. Walakini, katika maisha yake yote ya kazi hiyo, amekutana na tukio kama hilo mara moja tu.

Kwa mujibu wa Robert, kifo cha abiria kwenye ndege ni "tukio la nadra". Baadhi ya wafanyakazi wa ndege hawajawahi kukutana na tukio hilo wakiwa kazini angani.

Robert aliongeza kuwa watu wana uwezekano mkubwa wa kufa kwenye safari za ndege za masafa marefu kutokana na mwili kukaa sehemu moja kwa muda mrefu.

Jay Robert

Chanzo cha picha,Jay Robert

Maelezo ya picha,Robert amepitia mafunzo ya kukabiliana na vifo vya abiria angani.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la New England Journal of Medicine mwaka 2013 ulihitimisha kwamba vifo kwenye ndege ni tukio la "nadra." Lakini hutokea. Utafiti huo uliangalia simu za dharura kutoka kwa mashirika matano ya ndege kwenda vituo vya mawasiliano vya matibabu kati ya Januari 2008 na Oktoba 2010.

Ni 0.3% pekee ya wagonjwa wanaopata dharura za matibabu kwenye safari za ndege hufa, kulingana na utafiti.

Mwezi uliopita, wanandoa wa Australia Mitchell Ring na Jennifer Colin walielezea uzoefu "wa kutisha" wa kukaa karibu na mwili wa mwanamke kwenye ndege kutoka Melbourne hadi Doha.

Wafanyakazi wa ndege waliuweka mwili wa mwanamke huyo kwenye blanketi karibu na Ring kwa saa nne bila kujitolea kuusogeza.

Qatar Airways ilisema kuwa imefuata miongozo ifaayo na kuomba radhi kwa "usumbufu au huzuni yoyote ambayo tukio hili linaweza kusababisha", kwa abiria wengine.

d

Chanzo cha picha,Getty Images

BBC ilizunguza na wataalamu na wafanyakazi ndege kuhusu viwango vya kushughulikia vifo vinavyotokea angani.

Kando na kujadili sheria za kushughulikia miili kwenye ndege, waafanyakazi kadhaa walieleza uzoefu wao na kushughulikia vifo vya abiria.

Inaelezwa Wafanyakazi wa ndege hawawezi kuthibitisha kifo, hii ni lazima lifanywe na wafanyakazi wa sekta ya matibabu kama madaktari.

Ikiwa kuna wafanyakazi wa sekta hiyo kwenye ndege, basi uthibitisho wa kifo unaweza kufanywa na yeye. Hata hivyo, hilo mara nyingi hufanyika baada ya ndege kutua.

Mashirika mengi ya ndege hufuata miongozo ya Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA) kuhusu nini cha kufanya ikiwa abiria anashukiwa kufariki angani.

Kwa upande mwingine, sera zinaweza kutofautiana kidogo kati ya mashirika ya ndege.

Mwili kuwekwa kwenye kiti kisichokuwa na abiria

Katika tukio la dharura la matibabu, wafanyakazi wa ndege watatoa huduma ya kwanza wakati wakitafuta usaidizi kutoka kwa abiria wanaofanya kazi kama wafanyakazi wa matibabu, kwa maana ya madaktari na manesi.

Wakati huo huo, rubani wa ndege atatumia mfumo wa mawasiliano kupata maagizo kutoka kwa madaktari wa dharura waliopo chini namna ya kumuhudumia.

Mambo haya mawili yalielezwa na Marco Chan, rubani wa zamani na mhadhiri mkuu katika Chuo Kikuu Kipya cha Buckinghamshire.

Chan aliongeza kuwa marubani wanaweza kugeuza safari za ndege haraka iwezekanavyo ikiwa ni lazima, ili kuokoa maisha ya abiria.

Kwa bahati mbaya, mara nyingi ikitokea dharura angfani, juhudi za kuokoa maisha ya abiria hazifaulu mara zote kutokana na umbali na taratibu za kutua kwe nye viwanja vya dharula.

Pintu darurat

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Milango ya dharura yote kwenye ndege, lazima ipatikane na kutumika kwa urahisi

Ikiwa abiria atadhaniwa kuwa amekufa, macho yake lazima yafungwe na mwili wake lazima uwekwe kwenye begi maalumu la kuhifadhiwa mwili.

Kulingana na miongozo ya IATA, ikiwa begi la mwili halipo, ni lazima mwili ufunikwe hadi shingoni.

Nafasi kwenye ndege kawaida ni ndogo sana. Hii inafanya kuwa vigumu kwa wafanyakazi wa ndege kupata mahali pazuri pa kuweka mwili bila kusumbua abiria wengine na kuhatarisha usalama wa ndege.

Kulingana na miongozo ya IATA, miili inapaswa kuhamishwa hadi kwenye kiti kilicho mbali na abiria wengine au hadi eneo lingine la ndege kila inapowezekana.

Ikiwa ndege imejaa, mwili utawekwa kwenye kiti chake kile kile alichonunulia tiketi.

Kwenye ndege ndogo ambazo kwa kawaida hutumika kwa safari za masafa mafupi , hakuna nafasi ya kutosha, wakati mwingine hutumika mbinu ya "kuwaficha abiria kutokana na kile kinachoendelea".

Hii ilisemwa na Ivan Stevenson, profesa msaidizi wa usimamizi wa anga katika Chuo Kikuu cha Coventry.

"Iwapo mtu atakufa kwenye ndege kama hiyo, kuna uwezekano mkubwa atahitaji kuwekwa kwenye kiti," alisema.

Ingawa alikiri kwamba kuweka mwili kwenye kiti sio jambo la kupendeza kwa abiria wengine, Stevenson alisisitiza kwamba wafanyakazi wa ndege lazima watangulize suala la usalama wa ndege kwanza.

Kwa mujibu wa Jay Robert, wafanyakazi wa ndege "watajaribu kutoa heshima kwa mwili" kwa kuuweka mahala salama na kuuzungushia mapazia, blanketi na kupunguza taa.

Hata hivyo , Robert alikumbusha kwamba kwa kweli chaguzi za wafanyakazi wa ndege zinaweza kuwa ndogo huko angani.

Miili haiwezi kuwekwa jikoni ama katikati ya njia kwa sababu inaweza kuwa kizuizi iwapo litatokea jambo la dharura.

Miili pia haiwezi kuwekwa katika maeneo ya mapumziko ya wafanyakazi wa ndege hasa za masafa marefu.

Ilustrasi awak kabin

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Mmoja wa wahudumu wa ndege akiwa kazini

Kando na hayo, nafasi ndogo pia inafanya iwe vigumu kusogeza miili, alisema Robert.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa shirika la ndege la Qatar. Mitchell Ring alisema kuwa abiria waliokufa hawakuweza kuwekwa njiani.

Ndege hiyo itaelekezwa kuruma ilikotoka ili kuokoa maisha ya abiria iwapo kutatokea dharura ya kiafya. Htaa hivyo, hii haifanyiki ikiwa abiria anashukiwa kuwa amekufa.

"Hakuna maana katika kughairisha safari za ndege," Chan alisema.

Kkwa mujibu wa Profesa Stevenson, rubani atatoa taarifa mara moja kwenye kituo cha mawasiliano cha shirika husika la ndege na kituo cha mawasiliano ya ndege kwneye uwanja wa ndege kuhusu kifo cha abiria.

Wenye mamlaka na suala hilo watakuwa wakisubiri ndege itakapotua.

Ikiwa marehemu anasafiri kwenye ndege akiwa peke yake, mamlaka na wawakilishi wa shirika la ndege watawasiliana na familia inayohusika.

'Nililia bafuni'

Ally Murphy, mtangazaji wa kipindi cha 'Red Eye Podcast' ambaye mara nyingi huwahoji wahudumu wa ndege, alikumbana na kifo cha abiria mmoja wakati wa safari ya ndege katika miaka yake 14 kama mhudumu wa kabati.

Abiria wa kiume aliyekuwa akisafiri peke yake kutoka Accra, Ghana, kuelekea London alianguka kwenye kiti chake.

Baada ya kuarifiwa na abiria aliyekuwa kwenye kiti kilichokuwa karibu naye, wahudumu wa ndege hiyo waligundua kuwa alikuwa hapumui kawaida na hakuwa na mapigo ya moyo.

Wahudumu hao walimhamisha mtu huyo kwenye machela maalumu kwa ajili ya huduma ya kwanza (CPR).

Ally Murphy

Chanzo cha picha,Susan Doupé

Maelezo ya picha,Ally Murphy anaelezea kifo cha abiria kwenye ndege wakati akiwa kazini kuwa ni uzoefu 'mbaya'.

Kwa dakika 40, Murphy na muhudumu mwenzake walitoa huduma ya kwanza ya kushtua mapigo ya moyo (CPR) bila mafanikio.

Kisha rubani aliamua kuelekeza ndege hiyo hadi Lyon, Ufaransa. Ingawa Ally na mwenzake walijua kwamba walipaswa kufunga mikanda ili kutua, waliendelea kutoa huduma ya kwanza ya CPR.

"Hatutaki kuachana nayo," alisema.

Baada ya kutua, madaktari walitangaza kuwa mtu huyo alikuwa ameshakufa.

"Nilimshikilia katika dakika zake za mwisho za maisha," alisema.

"Mimi sio ndugu yake yake, lakini angalau hakuwa peke yake."

Baada ya kutua kwa dharura, ndege ilirudi angani na kuendelea na safari. Kwa mujibu wa Murphy, abiria walikuwa kimya na hali ilikuwa ya shwari.

Hata hivyo, mara tu walipotua tena kuna baadhi ya abiria walionyesha kukasirika na kulalamika baada ya kuchelewa ndege za kuunganisha kuendelea na safari zao.

"Ndio wakati pekee niliwaambia abiria wanipishe," Murphy alisema.

Kumuangalia abiria akikata roho lilikuwa tukio la kuhuzunisha kwa Murphy.

"Nilienda nyumbani, nikakaa bafuni, kisha nikalia. Bado ningeweza kufikiria pumzi ya mtu huyo kwa wiki moja," alisema.

"Niliumia sana. Kwa muda mrefu, sikuweza kutazama vipindi vya TV vilivyoonyesha matukio ya CPR.

Kulingana na Robert, wafanyakazi wa ndege wanapewa mapumziko ya muda baada ya kukutana na tukio kama hili kama ilivyokuwa kwa Murphy na wenzake.

Wafanyakazi wa ndege hawajazoea kushughulika na vifo vya abiria. Matukio kama yale ambayo Murphy alipitia yanaweza kuacha kumbukumbu mbaya sana.

"Sisi sio madaktari, sisi sio wauguzi," Jay Robert alisema.

"Ingawa tumefunzwa kukabiliana nayo, haimaanishi kuwa tuna kinga kwa sababu hili sio jambo tunalopitia kila siku."



Prev Post FOREMAN: Bondia aliyetajirika baada ya ngumi
Next Post Bodi ya EWURA yakagua bomba la mafuta TAZAMA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook