
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Kanali Mstaafu Dkt. Hassy Kitine, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Dkt. Kitine alizaliwa mwaka 1943 katika Kijiji cha Kisinga, Kata ya Lupalilo, Tarafa ya Lupalilo, Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe.
Katika historia ya uongozi wake, Dkt. Kitine aliteuliwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa wakati huo, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS kuanzia mwaka 1978 hadi 1980.
Kifo chake ni pigo kwa taifa, hasa katika sekta ya usalama na uongozi wa kitaifa, ambapo mchango wake uliacha alama isiyofutika katika taasisi nyeti za dola.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!