Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Burkina Faso yapitisha sheria kali dhidi ya uhusiano wa jinsia moja

  • 11
Scroll Down To Discover

Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso imepitisha sheria inayopiga marufuku uhusiano wa kimapenzi wa jinsi moja na kuweka adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitano jela, hatua ambayo inaiweka nchi hiyo miongoni mwa mataifa ya Afrika yaliyoanzisha sheria kali dhidi ya uhusiano huo unaohusisha ushoga.

Kabla ya hatua hii, uhusiano huu haukuwa umeharamishwa nchini Burkina Faso, lakini hali hiyo imebadilika tangu jeshi lilipochukua madaraka miaka mitatu iliyopita kufuatia mapinduzi ya mara mbili mwaka 2022.

Kulingana na tovuti ya Africainsider, muswada huo wa sheria ulipitishwa kwa kauli moja na wabunge 71 wa bunge la mpito lisilochaguliwa na wananchi.

“Sheria hii inaweka adhabu ya kifungo cha kati ya miaka miwili hadi mitano pamoja na faini,” amesema Waziri wa Sheria wa Burkina Faso, Edasso Rodrigue Bayala, kupitia televisheni ya taifa RTB.

Amesema kuwa raia wa kigeni watakaopatikana na makosa hayo watarudishwa makwao. Sheria hiyo pia ni sehemu ya mabadiliko mapana ya sheria za familia na uraia, na serikali imetangaza kuwa itasambazwa kwa wananchi kupitia kampeni za uhamasishaji.

Mataifa jirani yamechukua hatua kama hiyo; Mali, ambayo pia iko chini ya utawala wa kijeshi, ilipitisha sheria ya kuharamisha ushoga mnamo Novemba 2024. Ghana na Uganda pia zimeimarisha sheria zao dhidi ya ushoga katika miaka ya karibuni licha ya ukosoaji mkubwa wa kimataifa.

Nchini Uganda, sheria iliyopitishwa hivi karibuni imeweka kipengele cha “ushoga uliokithiri” kama kosa la adhabu ya kifo, huku makosa ya uhusiano wa ridhaa kati ya watu wa jinsi moja yakihusisha kifungo cha maisha jela.



Prev Post Dkt. Samia Kuendelea na Kampeni za CCM Leo Mkoani Songwe
Next Post Dkt. Nchimbi Amwomba Mpina Kurejea CCM, Aahidi kumpokea mwenyewe
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook