Wiki iliyopita mitandao ya kijamii ilivuma kwa picha zilizomuonesha Mtanzania, Issa Kwisa, ambaye alikuwa akiishi nchini Afrika Kusini, akidaiwa kuuawa na Polisi wa nchini humo katika mazingira ambayo bado hayajafahamika vyema.
Ili kufahamu undani wa tukio hilo, kituo cha Global TV kimefunga safari hadi nyumbani kwa wazazi wa marehemu maeneo ya Yombo Kilakala, Dar es Salaam, ambapo kilizungumza na mama mzazi wa kijana huyo, Bi. Joyce Adam.
Bi. Joyce ameeleza kwa uchungu kuwa taarifa za kifo cha mwanaye zilimfikia ghafla na zimeacha pengo kubwa katika familia. Amebainisha pia kuwa mazingira ya kifo hicho yanahusishwa na Polisi wa Afrika Kusini, ingawa bado hakuna ufafanuzi rasmi kutoka kwa mamlaka husika.
Aidha, familia ya marehemu imeomba serikali ya Tanzania na ubalozi wake nchini Afrika Kusini kufuatilia kwa ukaribu ili kujua ukweli wa kilichotokea na kuchukua hatua stahiki.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!