

Taifa la Kenya limegubikwa na huzuni kufuatia kifo cha Kadhi Mkuu wa Kenya, Sheikh Abdulhalim Hussein, ambaye alifariki dunia Jumatano, Julai 10, 2025, mjini Mombasa.
Taarifa za kifo chake zilitolewa na Sheikh Jamaludin Osman, Imamu wa Msikiti wa Jamia, kupitia tangazo rasmi lililosambazwa kwa waumini na umma.
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea. Ninasikitika kuwatangazia kifo cha Kadhi wetu Mkuu Sheikh Abdulhalim Hussein kilichotokea muda mfupi uliopita huko Mombasa. Atazikwa Mombasa,” alisema Sheikh Osman kwa masikitiko makubwa.
Historia na Mchango Wake kwa Taifa
Sheikh Abdulhalim aliteuliwa kuwa Kadhi Mkuu wa Kenya mnamo Julai 2023, akichukua nafasi ya Sheikh Ahmed Muhdhar aliyestaafu baada ya kuhudumu kwa miaka 12. Mchakato wa uteuzi wa Kadhi Mkuu uliongozwa na Tume ya Huduma za Idara ya Mahakama (JSC), na Sheikh Abdulhalim aliibuka kutoka miongoni mwa wagombea watano walioorodheshwa kwa nafasi hiyo ya juu kabisa ya kisheria kwa Waislamu nchini.
Katika nafasi hiyo ya kikatiba, Sheikh Abdulhalim alikuwa na jukumu muhimu katika kushughulikia masuala ya familia miongoni mwa Waislamu, ikiwa ni pamoja na: Masuala ya ndoa, Talaka, Urithi na Ushauri wa kifamilia kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu (Sharia)
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!