
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema imegundua mbinu mpya na ya kushtua inayotumika kuingiza dawa za kulevya nchini, ambapo wafanyabiashara haramu hutumia maiti kusafirisha kiasi kikubwa cha dawa hizo hatari.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema mamlaka hiyo imebaini kuwa mtandao wa biashara haramu ya dawa hizo sasa unatumia jeneza au miili ya marehemu kusafirisha dawa, hali inayohitaji umakini na ushirikiano mkubwa kutoka kwa taasisi mbalimbali na jamii kwa ujumla.
“Huu ni ujanja mpya wa kihalifu unaokusudia kukwepa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia njia ambazo awali hazikuhisiwa kabisa – ikiwa ni pamoja na jeneza au maiti.” — alisema Lyimo.
Kamishna Lyimo ameongeza kuwa uchunguzi unaendelea na tayari baadhi ya wahusika wameanza kuchukuliwa hatua, huku akitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa mamlaka pale wanapohisi jambo lisilo la kawaida.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!