

Rais wa Kenya, William Ruto, ameapa kuchukua hatua kali kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinarejea nchini, akisema yuko tayari kutumia mbinu zozote zinazohitajika kukomesha wimbi la maandamano ya hivi karibuni.
Akizungumza kwa hisia kali katika hafla ya uzinduzi wa makazi ya polisi jijini Nairobi, Rais Ruto alisema:
“Inatosha! Hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee. Tutatumia njia zozote kuhakikisha nchi inabaki salama na yenye utulivu.”
Kauli hiyo imekuja baada ya maandamano makubwa ya vijana – maarufu kama ‘Gen Z’ yaliyoanza mwezi Juni 2024, kupinga nyongeza ya kodi, lakini baadaye kugeuka kuwa wito wa mabadiliko ya kiutawala, ikiwa ni pamoja na:
Ruto ajiuzulu
Kukomeshwa kwa ukatili wa polisi
Kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali
Rais Ruto kwa mara ya kwanza amejibu kwa ukali maandamano hayo, akiwatuhumu wanasiasa wa upinzani kuhusika na kupanga mikakati ya kumng’oa madarakani:
“Ni viongozi wanaowafadhili vijana kutekeleza vitendo hivyo. Tunawafuatilia!”
Aliwaonya kuwa wanaotaka urais wa Kenya wasijifiche nyuma ya maandamano, bali wakutane naye 2027, wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!