Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wasomi UDSM Waja na Drone Kubwa Yenye Uwezo wa Kufanya Mambo Mbalimbali

  • 43
Scroll Down To Discover

Dar es Salaam 6 Julai 2025: Wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM katika Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ambayo yanachagiza bunifu mbalimbali mwaka huu kwenye Maonesho ya Kibiashara ya 49 ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar wamekuja na drone za kisasa ikiwemo yenye uwezo wa kubeba uzito wa zaidi ya kilo 50 kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali.

Hii ni drone kubwa ya kumwagilia dawa mashambani.

Akizungumza na Global Tv, rubani wa drone hizo, Imman Aloy Mchinja amesema zinaweza kutumika katika kazi mbalimbali ikiwemo kukagua usalama wa shambani, kumwagilia dawa za kuua wadudu na hata kubeba vitu mbalimbali kutoka sehemu moja ya shamba mpaka nyingine.

Rubani wa drone akielekeza jambo.

Rubani huyo amesema teknolojia ya kutumia drone hizo itawakomboa wakulima haswa wale waliokuwa wakivaa madumu mgongoni yenye dawa za kupulizia na kuua wadudu waharibifu ambao walikuwa wakifanya kazi hiyo kienyeji sasa wataifanya kisasa zaidi wakitumia drone hizo.

Ameendelea kusema kuwa kwa mkulima aliyekuwa na uwezo wa kupulizia dawa hizo ekari moja kwa siku sasa kupitia drone hizo ataweza kupulizia dawa kwa wadudu waharibifu kwa zaidi ya ekari 40 kwa siku na kumkomboa mkulima hivyo kujiongezea, amesema rubani huyo. HABARI/PICHA: NEEMA ADRIAN NA RICHARD BUKOS /GPL 



Prev Post Babalevo Amvaa Zitto Kabwe: “Kauli Yako Inadhalilisha Vipaji vya Wasanii” – Video
Next Post NMB YABEBA HUDUMA ZA BENKI HADI KWA MTEJA POPOTE ALIPO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook