Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TRA Yavunja Rekodi Kwa Kuvuka Malengo Ya Makusanyo Kwa Miezi 12 Mfululizo

  • 39
Scroll Down To Discover

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake kwa kuvuka malengo ya makusanyo kwa kila mwezi katika kipindi cha miezi 12 mtawalia (mfululizo). Katika mwaka wa fedha 2024/2025, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 32.26, sawa na ufanisi wa asilimia 103 ya lengo la Shilingi Trilioni 31.5, na ukuaji wa asilimia 16.7 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Akitoa taarifa hiyo kwenye hafla iliyofanyika tarehe 01 Julai 2025 jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema mafanikio hayo yametimia kupitia makusanyo ya robo ya nne ya mwaka, ambapo jumla ya Shilingi Trilioni 8.22 zilikusanywa, sawa na asilimia 104.8 ya lengo la Shilingi Trilioni 7.84 kwa kipindi hicho.

Bw. Mwenda amesema kiwango hicho ni ongezeko la asilimia 15.8 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 7.09 zilizokusanywa katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024. Aidha, ameeleza kuwa kwa miezi yote 12 ya mwaka wa fedha 2024/2025, TRA ilivuka malengo ya makusanyo – jambo ambalo halijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa Bw. Mwenda, wastani wa makusanyo ya kila mwezi umefikia Shilingi Trilioni 2.69 – kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa, kikiwa ni ongezeko kutoka Shilingi Trilioni 2.30 ya mwaka uliopita. Rekodi ya juu zaidi ya makusanyo kwa mwezi ni ya Desemba 2024 ambapo zilikusanywa Shilingi Trilioni 3.58, ikifuatiwa na Juni 2025 (Shilingi Trilioni 3.42) na Septemba 2024 (Shilingi Trilioni 3.02).

Kamishna Mkuu ameendelea kusema kuwa mafanikio hayo yamewezeshwa na ushirikiano mzuri baina ya walipakodi, viongozi wa serikali na watumishi wa TRA ambapo kwa kutambua mchango wao huo mkubwa, watumishi wote wa TRA walitumia dakika moja kusimama na kupiga makofi kuonesha heshima na shukrani kwa wote waliowezesha kufikiwa kwa mafanikio hayo.

“Nashukuru Mungu kwa kutuwezesha kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeniteua tarehe 02 Julai 2024 na kuniapisha tarehe 05 Julai 2024. Mhe. Rais, alinielekeza kuongeza makusanyo lakini pia kuimarisha mahusiano mazuri na walipakodi na kwa hakika tumefanikisha yote mawili; tumefikia malengo ya makusanyo, huku tukijenga uhusiano mzuri na walipakodi.



Prev Post Nilizika Mimba Tatu Bila Maelezo Lakini Baada ya Tiba ya Kiroho, Sasa Nimeshika Mimba Yangu ya Kwanza kwa Amani
Next Post IGP Wambura Awavisha Cheo Maafisa Watatu Waliopandishwa Cheo Na Rais Dkt. Samia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook