Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Liberia Kumzika Upya Rais wa Zamani William Tolbert Miaka 45 Baada ya Kuuawa

  • 54
Scroll Down To Discover

Rais wa zamani wa Liberia, William Tolbert, anatarajiwa kuzikwa upya Jumanne hii, ikiwa ni miaka 45 tangu auwawa katika mapinduzi ya kijeshi mwaka 1980, huku ikiaminika kuwa mwili wake ulitupwa kwenye kaburi la halaiki.

Tolbert aliuawa Aprili 12,  1980 wakati wa mapinduzi yaliyomuingiza madarakani Samuel Doe. Siku kumi baada ya kuuawa kwake, mawaziri 13 wa baraza lake la mawaziri walikamatwa na kushtakiwa kupitia kile kilichoitwa “mahakama ya kangaroo”. Mawaziri hao walipoteza nyadhifa zao, wakafungwa kwenye vigingi na kupigwa risasi hadi kufa kwenye ufukwe wa bahari karibu na kambi ya jeshi mjini Monrovia.

Kwa miongo kadhaa, hakuna maiti yoyote kati ya waliouawa iliyopatikana rasmi. Hata hivyo, sasa, kila mmoja miongoni mwa waliouawa anatazamiwa kupewa heshima ya mwisho kwa mazishi ya kitaifa katika hafla maalum itakayohudhuriwa na Rais wa sasa wa Liberia, Joseph Boakai, pamoja na viongozi wengine wa serikali na familia za waathirika.

Tukio hili linatazamwa kama ishara ya maridhiano ya kitaifa na sehemu ya juhudi za Liberia kukabiliana na historia yake ya vurugu na migogoro ya kisiasa. Ni hatua inayolenga kuponya majeraha ya kihistoria na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kupitia kumbukizi na heshima kwa waliopoteza maisha katika vipindi vya machafuko.



Prev Post Eric Shigongo Achukua Fomu Kuwania Ubunge Buchosa Kwa Muhula Wa Pili – Video
Next Post Mwanamke Alia Damu Baada ya Kugusa Picha ya Mpenzi Wake Mpya Kumbe Ni Mla Watu wa Kiroho    
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook