Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Yathibitisha Watanzania Walio Israel na Iran Wapo Salama

  • 5
Scroll Down To Discover

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitisha kuwa Watanzania waliopo katika mataifa ya Israel na Iran wako salama, licha ya hali ya taharuki iliyosababishwa na mashambulizi ya makombora kati ya nchi hizo kwa muda wa wiki moja iliyopita.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeelezwa kuwa juhudi za haraka zimeanzishwa kuhakikisha usalama wa raia hao, zikiwemo hatua za kuwaandaa kwa urejeshwaji salama nyumbani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali ya Tanzania inafanya kazi kwa ukaribu na Balozi zake zilizopo katika nchi za Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Kuwait na Israel, ili kuwaorodhesha Watanzania waliopo kwenye maeneo yaliyoathiriwa au yaliyo hatarini zaidi.



Prev Post Israel Yashambulia Tena Vituo Muhimu Vya Nyuklia Vya Iran
Next Post Serikali Yathibitisha Watanzania Walio Israel na Iran Wapo Salama
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook