Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kumekucha: Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Mara, Ajitosa Ubunge Kivule Dar

  • 26
Scroll Down To Discover

Mtia Nia Jimbo la Kivule Dar, Faustine Matiku (kushoto) akizungumza na wanahabari jijini Dar, leo alipokuwa akiwaeleza lengo lake na kutia nia kwenye jimbo hilo.
Dar es Salaam, 8 Juni 2025: Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini 2020 na kuambulia nafasi ya pili ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mara mpaka sasa, Faustine Matiku amejitokeza kutia nia ya kugombea ubunge Jimbo  la Kivule, Dar.
Wadau wakiwa makini kumsikiliza mtia nia, Faustine Matiku alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo, Matiku amesema ameamua kutumia fursa hiyo ya kugombea jimbo hilo jipya ambalo yeye kama mkazi wa eneo hilo na kuahidi kuanza kwa kuboresha maendeleo kwenye jimbo hilo jipya.
Baadhi ya mambo aliyosema ataanza nayo ni pamoja na kuboresha ufugaji wa kuku kisasa na kuanzisha soko la kisasa kwenye jimbo hilo ambalo wakazi wake wengi ni wajasiriamali wa biashara ya ufugaji na uuzaji wa kuku na mayai.
katika uboreshaji wa biashara hilo Faustine amesema atahakikisha wajasiriamali hao wanapata chakula cha mifugo yao pamoja na madawa kwa bei rafiki tofauti na ilivyo sasa wanavyouziwa kwa bei mbaya na kuwanyima faida kubwa.
Pamoja na hayo ameahidi kuboresha nyanja zingine za kimaendeleo kwenye jimbo hilo na kulifanya kuwa na maendeleo makubwa kuliko ilivyo sasa. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS/ GPL   



Prev Post Video: Majeruhi Aliyekuwa Ndani Ya Gari Iliyogongwa Na Watu 28 Kufariki Asimulia
Next Post Kumekucha: Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Mara, Ajitosa Ubunge Kivule Dar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook