Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Duma Boko: Tumaini Jipya la Botswana, Afata Nyayo za Traore – Video

  • 28
Scroll Down To Discover

Duma Gideon Boko, aliyefananishwa na viongozi wa kizazi kipya barani Afrika kama Ibrahim Traoré wa Burkina Faso, ameibuka kuwa kiongozi wa mabadiliko makubwa nchini Botswana.

Kama ambavyo Traoré ameongoza mapinduzi ya kisiasa na kiuchumi nchini kwake kwa kusimamia uhuru wa rasilimali na kupigania Afrika mpya, ndivyo Boko anavyoonyesha dira mpya ya maendeleo, haki na usawa katika taifa lake la Botswana.

Duma Boko alizaliwa tarehe 31 Desemba 1969 huko Mahalapye, Botswana. Alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Botswana, ambako alikuwa mwanaharakati wa haki za wanafunzi na mwanachama wa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi. Alionekana mapema kama mtu mwenye misimamo thabiti na aliyejitolea kwa haki za kijamii.

Baadaye alielekea Marekani na kusomea Shahada ya Uzamili ya Sheria (LL.M) katika Chuo Kikuu maarufu cha Harvard. Alirejea Botswana na kufundisha sheria ya katiba katika Chuo Kikuu cha Botswana kati ya mwaka 1993 hadi 2003, sambamba na kuendesha kampuni ya sheria iliyojikita katika kesi za maslahi ya umma.

Mwaka 2010, Boko alichaguliwa kuwa Kiongozi wa Botswana National Front (BNF), chama kikongwe cha upinzani. Aliongoza jitihada za kuunda umoja wa vyama vya upinzani uliojulikana kama Umbrella for Democratic Change (UDC) mnamo 2012. Umoja huo ulilenga kuvunja ukiritimba wa kisiasa wa Botswana Democratic Party (BDP) ambayo ilikuwa imeongoza tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1966.

Boko alihudumu kama Kiongozi wa Upinzani katika Bunge la Taifa kuanzia 2014 hadi 2019. Ingawa alishindwa katika chaguzi za urais za 2014 na 2019, hakukata tamaa. Alijenga mtandao mkubwa wa kisiasa, aliimarisha umoja wa vyama vya upinzani na kufanikisha ushindi mkubwa katika uchaguzi wa 2024.

Katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2024, muungano wa UDC chini ya uongozi wa Duma Boko ulipata viti 36 kati ya 61 vya Bunge la Taifa, na hivyo kumpatia nafasi ya kuwa Rais wa sita wa Botswan.



Prev Post Inatisha! Msoto Wa Watanzania India – Sarah Asimulia ”Wanajifungua Wanauza Watoto”- Video
Next Post Duma Boko: Tumaini Jipya la Botswana, Afata Nyayo za Traore – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook