Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CCM Yatangaza Ratiba ya Uchukuaji Fomu ya Dk. Hussein Mwinyi

  • 3
Scroll Down To Discover

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuchukua fomu ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) mnamo Agosti 30, 2025.

Hayo yalisemwa jana mjini Unguja na Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema majira ya saa 4 asubuhi, Dk. Mwinyi atafika katika ofisi za ZEC Maisara, mjini Unguja, kwa ajili ya kuchukua fomu. Baada ya hapo, mgombea atapanda gari maalum la wazi na kupita katika maeneo mbalimbali ya mjini Unguja.

Kwa mujibu wa Mbeto, Dk. Mwinyi atapita barabara ya Kwa Raju Magere, kisha Miembeni, na baadaye kupandisha barabara ya Mapinduzi Square kuelekea katika Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui, mjini Unguja.

Alisema atakapofika katika ofisi za chama, mgombea atashuka na kwenda kupata dua kwenye kaburi la Hayati Mzee Abeid Amani Karume. Baada ya hapo ataingia ndani ya ofisi za CCM kwa ajili ya kuzungumza na wazee na kusaini kitabu cha wageni.

Mbeto aliongeza kuwa, baada ya kutoka hapo, Dk. Mwinyi ataelekea katika viwanja vya Mau ambako kutafanyika shughuli za kuhitimisha hafla hiyo ya uchukuaji wa fomu.

Aidha, alibainisha kuwa Dk. Mwinyi atapata nafasi ya kuwahutubia wananchi wa Zanzibar na kueleza muelekeo wake wa miaka mitano ijayo kuhusu nini atawafanyia wananchi wa Zanzibar.

“Kwa maana hiyo, wananchi wote watakaomsindikiza mgombea barabarani, watatakiwa kuelekea katika viwanja vya Mau ambapo ndipo shughuli mbalimbali zitakapoendelea,” alisema.

Mbeto alitoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla kujitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea wao.



Prev Post Vodacom Yazindua Ripoti Ya ESG
Next Post NAFASI Za Kazi Karafu Enterprises LTD
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook