Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mahakama Kuu Yaahirisha Hukumu ya Shauri la Kikatiba la Mpina hadi Oktoba 15

  • 10
Scroll Down To Discover

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dodoma, imeahirisha kutoa hukumu katika shauri la kikatiba namba 24027 la mwaka 2025, linalohusu mwanachama wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, aliyepinga kuondolewa kwenye orodha ya wagombea wa urais.

Awali hukumu ilikuwa imetajwa kutolewa Oktoba 10, 2025, lakini sasa imesogezwa hadi Oktoba 15, 2025, majira ya saa 3:00 asubuhi, kwa njia ya mtandao.

Shauri hilo linasikilizwa na Jopo la Majaji Watatu likiongozwa na Jaji Frederick Mayanda, ambaye amesema kuwa hukumu bado haijakamilika, jambo lililosababisha kuahirishwa kwa tarehe ya kutoa uamuzi.

Akizungumza na wanahabari, Wakili wa waleta maombi, John Seka, aliwahimiza wananchi na wanachama wa ACT-Wazalendo kuwa na subira, akisisitiza kuwa wana imani kwamba Mahakama itatenda haki.

“Tunawaomba wanachama wetu na wananchi kuendelea kuwa na subira. Tuna imani kuwa Mahakama Kuu itatenda haki ipasavyo,” alisema Wakili Seka.

Shauri hili limeibua shauku kubwa kutokana na umuhimu wake katika mchakato wa uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025.

“HATUTAKAA KIMYA HADI MWISHO – WANATAKA KUTUNYAMAZISHA KILAZIMA” – HECHE ACHAFUKA NYONGO MAHAKAMANI




Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO OKTOBA 11, 2025
Next Post Rais Tshisekedi Awataka Waasi wa M23 Kujiondoa Mara Moja Mashariki mwa DRC
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook