
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 15 May 2025
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 15 May 2025
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Kuwa malengo ya Simba ni kutwaa kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) na wanakwenda kwenye mechi mbili za Fainali dhidi ya RS Berkane wakiwa na kauli mbiu ya TUNABEBA.
May 17 Simba itakuwa Morocco kucheza Fainali ya kwanza itakayopigwa uwanja wa Manispaa ya Berkane na mchezo wa marudiano utapigwa jijini Dar es salaam May 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika mkutano na wanahabari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali alisema kuwa wanasimba wanapaswa kuwa tayari na kila mmoja afahamu safari hii Simba inabeba kombe la Shirikisho baada ya kulikosa mwaka 1993 ilipocheza fainali wakati huo likiitwa kombe la CAF.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!