

Mama mmoja mwenye umri wa miaka 61, mkazi wa Kijiji cha Gedamara, wilayani Babati, mkoani Manyara, amedai kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, katika tukio lililotokea Januari 26 mwaka huu, nyumbani kwake Gedamara.
Kwa mujibu wa maelezo ya mama huyo, kijana huyo anayefahamika kwa jina la Luka alifika nyumbani kwake akiomba chakula, na baada ya muda alianza kufanya jaribio la kumbaka, jambo lililomlazimu mama huyo kujaribu kujihami. Katika harakati hizo, kijana huyo alidaiwa kumshambulia kwa kutumia mpini wa jembe, na kumpiga kichwani pamoja na kumvunja mguu mmoja.
Huyu ni mwanaye ambaye anasimulia tukio zima.
Ripota wa Global TV, @hoseaelnino, ametuletea simulizi kamili kutoka Gedamara.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!