
Leo Mei 8, 2025 moshi mweusi umetoka kwenye bomba la paa la Sistine Chapel ishara wazi kwamba Makardinali 133 bado hawajafikia muafaka juu ya nani atakayekuwa Papa wa 267 wa Kanisa Katoliki.
Hii ni sehemu ya mchakato wa Conclave unaofanyika kwa siri kubwa, ambapo kura hupigwa mara mbili kila siku hadi mmoja wa makardinali apate theluthi mbili ya kura zote.
Moshi mweusi unasemwa kuwa ujumbe wa kusubiri zaidi lakini pia wa matumaini kwamba kwa uvumilivu, mwangaza wa moshi mweupe utawasili hatimaye.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!