
Rihanna na A$AP Rocky wamethibitisha kuwa wanatarajia mtoto wao wa tatu. Taarifa hii imejulikana rasmi katika usiku wa Met Gala 2025, ambapo Rihanna alionekana akiwa mjamzito kwa mara ya kwanza hadharani. Muonekano wake katika tukio hilo kubwa la mitindo ulimvutia wengi, huku mashabiki na vyombo vya habari wakigundua wazi dalili za ujauzito.
Zaidi ya hapo, A$AP Rocky alithibitisha taarifa hizo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akipita kwenye Blue Carpet ya Met Gala. Alipohojiwa kuhusu hali ya Rihanna na uwezekano wa mtoto mwingine, alijibu kwa uthibitisho na tabasamu, akionyesha furaha yao kama wanandoa wanaotarajia kuongeza mtoto mwingine katika familia yao.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!