Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wafanyabiashara wa jengo lililoanguka Kariakoo wafungua kesi kudai fidia

  • 40
Scroll Down To Discover

Takriban Wafanyabiashara 50 wa ghorofa lililoanguka Kariakoo mwishoni mwa mwaka 2024 wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam ili kudai fidia kwa waliokuwa wamiliki wa jengo hilo.

Kesi hiyo ya Ardhi namba 6075 ya mwaka 2025, itasikikizwa Mahakamani hapo leo Aprili 29, 2025 mbele ya Jaji Mohammed Gwae.

Wakili Peter Madeleka amesema wafanyabiashara hao wanaamini kuwa kuanguka kwa jengo hilo kumesababishwa na uzembe uliofanywa na wamiliki wa jengo, na kupelekea athari kubwa ikiwemo kupoteza mali zao pamoja na makumi ya watu kupoteza maisha.

TAKUKURU yaokoa bilioni 9 mwaka 2024/2025

Wakili Madeleka ameongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa kesi ya jinai inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu waliyofunguliwa wamiliki hao, amesema kesi hiyo haitoshi kwa wafanyabiashara hao kurudi katika nafasi zao za awali, akiongeza kuwa kesi hiyo pia ni fundisho kwa wamiliki wa majengo ili kujali usalama wa maisha na mali za wafanyabiashara.

Katika tukio hilo la Novemba 16 mwaka jana, watu 31 walipoteza maisha na wengine 71 waliokolewa na kupatiwa matibabu.

The post Wafanyabiashara wa jengo lililoanguka Kariakoo wafungua kesi kudai fidia appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Wafanyabiashara wa jengo lililoanguka Kariakoo wafungua kesi kudai fidia
Next Post Fahamu Papa mpya anavyochaguliwa na Makadinali Vatikani Roma
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook