Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tanzania ni Nchi Huru, Salama Hatuna Mgogoro wa Kisiasa

  • 15
Scroll Down To Discover

•Chini ya uongozi wa Rais Samia nchi imetulia

DAR ES SALAAM: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka watanzania kusimama na Rais Samia Suluhu Hassan katika kulinda amani iliyopo nchini kwani Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine.

Pia kimesema Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia hakuna mgogoro wowote wa kisiasa na mtu yoyote na ni nchi iliyojaa uhuru na amani ambayo imekuwa mfano kwa mataifa mengine yanajifunza kupitia Tanzania.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla alieleza hayo leo Aprili 28,2025 wakati akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Ubungo Dar es salaam akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.


“Tanzania yetu ni salama Tanzania hii tutapishana kwa itikadi lakini hatuna Tanzania mbadala ni hii hii tunayoitegemea na chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan nchi yetu ni tulivu na nchi nyingine zinajifunza Tanzani,” amesema Makalla.

Pia amesema katika kipindi cha uchaguzi yatasikika mengi lakini amewataka wananchi waendelee kuwa wamoja na kuhubiri amani nchini kote, akisisitiza waachane na viongozi wenye siasa za uchochezi na za uchonganishi katika kipindi hiko.

Aidha, Makalla amesisitiza hakuna Tanzania nyingine mbadala na kwa kulitambua hilo kuelekea katika kipindi cha uchaguzi na wakati uchaguzi ukiendelea wanasiasa watapishana kwa itikada lakini wakiendela kulinda amani.

Ameongeza wanasiasa wanatakiwa kuja na hoja watakazoziwasilisha na kuzinadi kwa wananchi na katika wakati wa uchaguzi wananchi ndo wataamua chama gani wakichague na baada ya uchaguzi atakayeshinda atatangazwa kuwa mshindi na kupewa ridhaa ya kuongoza.

“Niwaombe watanzania waotufuatilia huu ni mwaka wa uchaguzi ni mwaka ambao kila chama kinakuja na ilani na muelekeo wake kitawapelekea wananchi na ndiyo watakaoamua chama gani wakichague na baada ya uchaguzi kitapewa ridhaa ya kuongoza,” amesema Makalla.

Pia Makalla amesema amefurahishwa na hotuba ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa dini zote kwa kuhubiri amani wakionesha imani yao juu ya uchaguzi, kwani upo kwa mujibu wa katiba na CCM watafanya kama walivyoeleza ili kulinda amani.



Prev Post Kesi ya Tundu Lissu Yasogezwa Mbele, Mwanasheria Mkuu wa Chadema Azungumza
Next Post Saifee Yaandaa Marathon Kuongeza Uelewa Kuhusu Magonjwa ya Moyo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook