Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Taifa Stars Yatangaza Kikosi cha Mechi Mbili Dhidi ya Nigeria

  • 7
Scroll Down To Discover

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Miguel Gamondi, ametangaza kikosi cha wachezaji kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) dhidi ya Nigeria.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo hiyo Novemba 13 na Novemba 17, 2026, huku kikosi hicho kikiwa na wachezaji wanaocheza ndani na nje ya Tanzania.

Katika kikosi hicho, wachezaji wanaotoka katika klabu za ndani ni pamoja na Aishi Manula, Zuberi Foba na Abdul Hamisi wa Azam FC, Himid Mao na Feisal Salum wa Azam SC, pamoja na Ibrahim Abdulla, Dickson Job, Bakari Mwannyeto, Seleman Mwalimu na Clement Mzize wa Yanga SC.

Wengine ni Anthony Mligo na Nathaniel Chilambo wa Simba SC, Evastus Lukanima wa Kagera Sugar na Sheikhan Khamis wa Singida Black Stars.

Kwa upande wa wachezaji wanaokipiga katika klabu za nje, kikosi hicho kinajumuisha Abdallah Hamisi anayeichezea Al Ain SC ya UAE, Haji Mnoga wa Patro Eisden ya Ubelgiji, Novatus Miroshi wa Göztepe ya Uturuki na Alphonse Mabula wa JS Kabylie ya Algeria.

Wengine ni Ben Starkie wa Truro City ya Uingereza, Simon Msuva wa Newroz SC ya Iraq, Kibu Denis wa Al Nasr ya Libya, Charles M’Mombwa wa Zabbar ya Malta, Cyprian Kachwele wa FC Kryvbas ya Ukraine na Bernard Kamungo wa FC Dallas ya Marekani.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza maandalizi chini ya kocha Miguel Gamondi kwa ajili ya michezo hiyo miwili muhimu katika harakati za Tanzania kuwania nafasi ya kushiriki AFCON 2027.

The post Taifa Stars Yatangaza Kikosi cha Mechi Mbili Dhidi ya Nigeria appeared first on Global Publishers.



Prev Post Kijana Javits Frimpong Aliyeuawa kwa Risasi Marekani Aamsha Hasira za Ubaguzi
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA MOSI, 2026 
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook