
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe, amemfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
Mbowe alifika nyumbani kwa Rais Samia, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 10, 2026, ambapo alitoa pole na kumfariji Rais Samia katika kipindi hiki cha majonzi.
Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Ujio wa Mbowe Kizimkazi ni sehemu ya viongozi na watu mbalimbali wanaofika kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo.
Katika kipindi hiki cha maombolezo, Rais Samia amekuwa akipokea salamu za rambirambi na pole kutoka kwa viongozi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, huku ndugu, marafiki na wananchi wakiendelea kuungana naye katika kipindi hiki kigumu.
Maalim Hafidh Ameir Hassan ataendelea kukumbukwa kwa nafasi yake katika familia na jamii, huku msiba wake ukiwa umewagusa watu mbalimbali waliokuwa karibu na familia hiyo.

The post Mbowe Amfariji Rais Samia Kizimkazi Baada ya Kufiwa na Mumewe appeared first on Global Publishers.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!