Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Matajiri wa Jiji Azam Fc na Namungo Kukipiga Leo Ligi Kuu ya NBC

  • 2
Scroll Down To Discover

Klabu ya Azam FC leo Jumatatu, Septemba 7, 2026, inashuka dimbani kumenyana na Namungo FC katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji alama tatu muhimu ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi.

Kwenye msimamo kuelekea mtanange wa leo, timu hizi zinapishana kwa pointi na nafasi, kulingana na mwanzo wao wa msimu wa 2026/2027.

Azam FC,imecheza mechi tano,  inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 11.

Azam FC inalenga kupata ushindi leo ili kuisogelea Yanga SC na Simba SC zilizopo kileleni mwa msimamo, kila moja ikiwa na pointi 15.

Namungo FC kwa upande wao, imecheza mechi tano, lakini inasuasua kwenye msimamo ikiwa na pointi tatu pekee.

Na Peter Jinanai

The post Matajiri wa Jiji Azam Fc na Namungo Kukipiga Leo Ligi Kuu ya NBC appeared first on Global Publishers.



Prev Post Makamu wa Rais Ndejembi Aungana na Waombolezaji Maziko ya Hafidh Ameir Hassan (Video +Picha)
Next Post Infantino Athibitisha Kugombea tena Urais wa FIFA Mwakani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook