
Unamkumbuka mwanadada Agnes Masogange aliyetangulia mbele za haki? Huyu hapa ni mwanaye ambaye amehitimu kidato cha sita.
Global TV imefika kwenye mahafali yake ambapo mwanadada Wolper aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu, alifika kujumuika na mtoto huyo.
Binti huyo amehitimu katika Shule ya Sekondari ya Patric Mission iliyopo Mivumoni, Madale jijini Dar es Salaam, ambapo mkurugenzi wa shule hiyo Ndele Mwaselela ndiye aliyemsimamia tangu mama yake alipofariki dunia.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!