Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Afanya Mabadiliko, Ateua CEO wa TAFICO na Balozi Malaysia

  • 11
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili katika sekta ya uvuvi na diplomasia, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utendaji wa taasisi za umma na uwakilishi wa nchi nje ya mipaka yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua Dkt. Suleiman Peter Kiula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).

Dkt. Kiula anachukua nafasi ya Bw. Shaibu Ramadhan Matessa, ambaye ameondolewa katika nafasi hiyo na atapangiwa majukumu mengine ya serikali.

Katika uteuzi huo huo, Rais Samia amempangia Balozi Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia, ambako ataiwakilisha Tanzania katika masuala ya kidiplomasia na ushirikiano wa kimataifa.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, tarehe 6 Agosti 2026.

The post Rais Samia Afanya Mabadiliko, Ateua CEO wa TAFICO na Balozi Malaysia appeared first on Global Publishers.



Prev Post Polisi Wavunja Ukimya Kuhusu Sanduku Lililotelekezwa Mwenge – Video
Next Post Malkia wa Matumaini TikTok Afariki Akiwa na Miaka 26, Familia Yake Yafunguka
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook