Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Marekani na Iran Wakubaliana Kusitisha Vita kwa Siku 60

  • 12
Scroll Down To Discover

Marekani na Iran zimefikia makubaliano ya awali ya kuongeza muda wa usitishaji mapigano huku zikisubiri idhini ya Rais wa Marekani Donald Trump, kwa mujibu wa ripoti ya Axios.

Makubaliano hayo yamekuja baada ya Iran kushambulia kambi ya jeshi la Marekani nchini Kuwait siku ya Alhamisi, kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya kile Washington ilichodai kuwa ni operesheni ya droni za Iran.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, pande hizo mbili zimekubaliana memorandum ya siku 60 itakayoongeza muda wa usitishaji vita na kufungua mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, ingawa mpango huo bado unasubiri uamuzi wa mwisho wa Trump.

“Haya ni makubaliano ya kuwarudisha wote mezani kwa mazungumzo. Tutaweka wazi maelezo yote wakati wa majadiliano,” amesema mmoja wa maafisa wa Marekani.

Afisa mwingine wa Marekani amesema Rais Trump amewasilisha ujumbe kwa wapatanishi kuwa anahitaji siku chache kutafakari kabla ya kutoa uamuzi wake rasmi.

Bei za mafuta duniani zilishuka baada ya taarifa hiyo kutoka, huku wachambuzi wakisema mashambulizi ya hivi karibuni yanaonyesha namna mazungumzo hayo yalivyo dhaifu licha ya matumaini ya kugeuza usitishaji huo wa mapigano kuwa makubaliano ya kudumu.

Mvutano huo umeendelea kuathiri eneo muhimu la usafirishaji wa mafuta la Hormuz, ambalo ni moja ya njia muhimu zaidi za biashara ya mafuta duniani.

The post Marekani na Iran Wakubaliana Kusitisha Vita kwa Siku 60 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Wanafunzi 16 wafariki katika moto wa bweni la shule nchini Kenya, katika Dira ya Dunia TV
Next Post Mashabiki wa Tyla Wapaniki Baada ya Kutoweka Mitandaoni Kabla ya APop
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook