Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Mwigulu Afanya Mazungumzo na Rais wa AfDB

  • 16
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika Jumanne Mei 26, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele (Kintele Congress Centre) jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na taasisi hiyo.

Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika pamoja na wadau wa maendeleo kujadili masuala ya uchumi, uwekezaji na maendeleo ya bara la Afrika.

The post Waziri Mkuu Mwigulu Afanya Mazungumzo na Rais wa AfDB appeared first on Global Publishers.



Prev Post Tinubu Ashinda Uteuzi wa APC Kugombea Urais Nigeria 2027
Next Post Mama Mzazi wa Hayati Magufuli Kuzikwa Ijumaa Chato, Serikali Kugharamia Mazishi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook