Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

PSRS Yatangaza Nafasi za Kazi 309 – Chuo Ushirika Moshi, TRC, eGA, ARU na Nyingine

  • 14
Scroll Down To Discover

Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza rasmi nafasi kubwa za ajira 309 katika taasisi mbalimbali za serikali na mashirika ya umma nchini Tanzania.

Tangazo hilo linahusisha nafasi za kazi katika taasisi kama vile Mzumbe University (MU), Ardhi University (ARU), Moshi Co-operative University (MoCU), e-Government Authority (eGA), Tanzania Railways Corporation (TRC), Tanzania Government Flight Agency (TGFA) na National Arts Council (NAC) pamoja na taasisi nyingine za umma.

Fursa hizi mpya za ajira zinahusisha kada mbalimbali zikiwemo:

  • ICT Officers katika maeneo ya Programu, Mitandao, Database na Helpdesk
  • Wahandisi, Mafundi na Wataalamu wa Ufundi
  • Madereva, Wasaidizi wa Ofisi na Mapokezi
  • Wataalamu wa Reli, Anga na Usafirishaji
  • Wataalamu wa Sanaa na Utamaduni

PSRS imesisitiza kuwa waombaji wote wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mfumo rasmi wa ajira wa serikali kupitia http://portal.ajira.go.tz kabla ya tarehe ya mwisho ya 01 Juni 2026.

Waombaji wanakumbushwa kuwasilisha nyaraka sahihi, zikiwemo vyeti vya elimu, kitambulisho cha taifa (NIDA), na taarifa nyingine muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo rasmi.

PSRS imeeleza kuwa waombaji wote wenye sifa wanahimizwa kuchangamkia fursa hii adimu ya ajira serikalini, huku ikisisitiza kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo rasmi hayatazingatiwa.

MUHIMU:

Mwisho wa kutuma maombi: 01 Juni 2026

ERIC SHIGONGO – “HATUKATAI WAGENI – WASIJE KUUZA NYANYA SIYO WAGENI TUNAOWATAKA – WAZAWA WALINDWE”

The post PSRS Yatangaza Nafasi za Kazi 309 – Chuo Ushirika Moshi, TRC, eGA, ARU na Nyingine appeared first on Global Publishers.



Prev Post Video: Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Awaka Kisa Matukio ya Utekaji Nchini
Next Post Trump Afunguka Ugumu wa Kuhudhuria Harusi ya Mwanaye Katika Kisiwa cha Bahamas
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook