
Rio Ferdinand, nahodha na mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza pamoja na Klabu ya Manchester United, leo Mei 20, 2026 ametembelea viunga vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma kwa ajili ya kushuhudia shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Bunge hilo.

Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa safari yake nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha sekta ya michezo pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.
Katika ziara hiyo, Rio Ferdinand amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ambaye alikuwa mwenyeji wake katika shughuli hiyo muhimu.




The post Rio Ferdinand Atembelea Bunge la Tanzania Katika Ziara ya Michezo na Utalii appeared first on Global Publishers.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!