Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Filamu ya #NotiFeki Yatoa Tahadhari kwa Mawakala wa Miamala – Video

  • 25
Scroll Down To Discover

Wafanyabiashara wa huduma za miamala ya simu nchini, maarufu kama mawakala, wameendelea kuwa miongoni mwa waathirika wakubwa wa matukio ya utapeli yanayoongezeka kila siku, hasa katika maeneo ya mijini.

Kutokana na hali hiyo, Global TV kwa kushirikiana na Hash Power Films wameandaa filamu fupi iitwayo #NotiFeki, inayolenga kuonesha mbinu mbalimbali zinazotumiwa na matapeli kuwaibia mawakala wa miamala ya simu.

Filamu hiyo ni sehemu ya kwanza ya mfululizo wa kazi maalum za uhalifu zinazofanyika ndani ya Jiji la Dar es Salaam chini ya jina la #CrimeinDarCity, ikiwa na dhamira ya kutoa elimu kwa jamii kupitia simulizi zinazoakisi matukio halisi yanayotokea mitaani.

Kupitia #NotiFeki, watazamaji watapata nafasi ya kuona namna baadhi ya matapeli wanavyotumia ujanja, haraka na mazingira ya biashara kuwahadaa mawakala na kutoweka na fedha zao bila kugundulika mapema.

Waandaaji wa kazi hiyo wamesema lengo si burudani pekee, bali pia kuongeza uelewa kwa wananchi na wafanyabiashara kuhusu tahadhari wanazopaswa kuchukua wanapofanya shughuli za kifedha kila siku.

“TAIFA HALITAJENGWA KWA UNAFIKI-TUNAHITAJI WATANZANIA WALIO HURU KUTOA MAWAZO”-MANENO YA DKT NCHIMBI

The post Filamu ya #NotiFeki Yatoa Tahadhari kwa Mawakala wa Miamala – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post KAMWE AAMINI DUBE ATAIBEBA YANGA KUTETEA UBINGWA
Next Post USM Alger Yabeba Ubingwa Kombe la Shirikisho kwa Mara ya Pili, Che Malone Aandika Historia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook