Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Kombo Amwakilisha Rais Samia Katika Uapisho wa Rais Guelleh Djibouti

  • 20
Scroll Down To Discover

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Djibouti Mhe. Ismaïl Omar Guelleh, zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Djibouti ulioko jijini Djibouti.

Pia Mheshimiwa Waziri Mahamod Thabit Kombo amewasilisha Ujumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Djibouti Mhe. Ismaïl Omar Guelleh.

Rais Ismaïl Omar Guelleh amechaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa sita mfululizo kufuatia ushindi alioupata kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Aprili 10, 2026.

Rais Guelleh mwenye umri wa miaka 78, amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 27 sasa akiliongoza taifa hilo dogo la Pembe ya Afrika lenye watu takribani milioni moja.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Kombo baada ya sherehe za uapisho alimkabidhi Rais Guelleh ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sherehe hizo za uapisho zimehudhuriwa na Wakuu wa nchi mbalimbali kutoka Ethiopia, Somalia, Sudan Kusini, Gabon na Yemen, pamoja na viongozi wengine mbalimbali waliowawakilisha wakuu wa nchi zao.

Akihutubia baada ya kuapishwa, Mheshimiwa Rais Guelleh amewashukuru wananchi wa Djibout kwa imani na heshima kubwa waliyompatia na akaahidi kuboresha mifumo ya Elimu, kukuza uchumi na teknolojia, kuimarisha usalama wa kikanda na kuongeza ajira.

Akizungumza baada ya sherehe hizo, Mheshimiwa Waziri Kombo amempongeza Rais Guelleh kwa ushindi aliopata na kumtakia heri katika kuwatumikia wananchi wa Djibouti ambao wameonyesha imani kubwa kwake.

Aidha Mheshimiwa Kombo amesema Tanzania na Djibouti ni nchi marafiki wa muda mrefu wenye uhusiano mzuri na kutoa rai kwa wananchi wa Tanzania na Djibouti kuhakikisha wanauendeleza urafiki huo kwa manufaa wa wananchi wa pande zote mbili.

The post Waziri Kombo Amwakilisha Rais Samia Katika Uapisho wa Rais Guelleh Djibouti appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Mkuu Aeleza Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita Kwenye Michezo
Next Post Oryx Energies Yapewa Hongera Kwa Kuunga Mkono Nishati Safi ya Kupikia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook