Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Apewa Tuzo na BMT Kutambua Mchango Wake Kwenye Michezo

  • 21
Scroll Down To Discover

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amekabidhi Tuzo Maalum ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa Waziri Mkuu, Mwigulu Lameck Nchemba, ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa Rais huyo katika maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika hafla ya Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) 2025 zilizofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, ambapo wadau mbalimbali wa michezo walihudhuria kushuhudia tukio hilo la heshima.

Tuzo hiyo maalum imetolewa kama ishara ya kutambua juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha na kuwekeza katika sekta ya michezo, hatua ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa ushindani na mafanikio ya wanamichezo wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

Katika hafla hiyo, viongozi mbalimbali wa serikali, wanamichezo na wadau wa michezo wameendelea kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kupitia uwekezaji na sera zilizowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya michezo.

MAMA ALIA kwa UCHUNGU KISA SHIDA ya MAJI GEITA – ”TUMECHOKA – KAMFIKISHIENI HII RAIS SAMIA”…

The post Rais Samia Apewa Tuzo na BMT Kutambua Mchango Wake Kwenye Michezo appeared first on Global Publishers.



Prev Post YANGA YAKIRI SIMBA IMEBADILIKA, KAMWE AFUNGUKA UKWELI MZITO
Next Post Waziri Mkuu Aeleza Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita Kwenye Michezo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook