Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

ALIYEIPA SIMBA ALAMA MOJA KARIAKOO DERBY AVUNJA UKIMYA

  • 12
Scroll Down To Discover

BEKI wa Yanga SC, Israel Mwenda, amekiri hadharani kufanya kosa kazini lililoigharimu timu yake katika mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC uliomalizika kwa sare ya 2-2.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Mwenda aliamua kusema ukweli mchungu kwa mashabiki wa Wananchi, akichukua lawama zote kwa matokeo ya mchezo huo.

Kwa masikitiko makubwa, Mwenda aliweka ujumbe uliogusa hisia za wengi, amesisitiza kuwa hatotafuta kisingizio chochote kwa yaliyotokea uwanjani.

“Siku na siku nzuri kazini nimekosea na kuigharimu timu, nimewaangusha wachezaji wenzangu na mashabiki na nipo tayari kupokea lawama zote kutoka kwa mashabiki, ishara ya ukomavu na uwajibikaji,” amesema Mwenda.

Beki huyo ameonyesha kuumizwa na namna juhudi za Wananchi zilivyokwenda bila malipo kwenye pambano hilo la watani wa jadi dimbani Mbweni.

“Wananchi hamkustahili kuona juhudi zenu na sapoti zikiishia bila furaha,” amesema Mwenda.

Licha ya maumivu ya kuikosesha timu yake ushindi, Mwenda hakukata tamaa, ameahidi kujifunza kutokana na kosa hilo na kurejea akiwa na makali zaidi.

“Nimejifunza kwa makosa na ntapambana zaidi kurudi nikiwa bora kuliko leo,” amesema beki huyo .

The post ALIYEIPA SIMBA ALAMA MOJA KARIAKOO DERBY AVUNJA UKIMYA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIRI YA UBABE WA YANGA YAFICHUKA, PEDRO AMESEMA NIDHAMU SILAHA YAO
Next Post Beyoncé Ang’ara Met Gala 2026 Arudi Kwa Kishindo Baada Ya Miaka 10
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook