Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Wachunguza Kifo cha Mtu Aliyekutwa Bila Kichwa Mto Msimbazi – Video

  • 29
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa kifo cha mtu ambaye mwili wake ulikutwa ukielea katika maji ya Mto Msimbazi, eneo la Kipawa wilayani Ilala.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polisi, tukio hilo lilitokea Aprili 30, 2026 majira ya saa 9:00 alasiri, ambapo mwili huo ulionekana ukielea katika maji yaliyokuwa yakitiririka mtoni humo.

Ilielezwa kuwa mwili huo haukuwa na kichwa, hali iliyozua maswali na kuongeza uzito wa uchunguzi unaoendelea.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa huenda mwili huo ni wa mtu aitwaye James Temba, mkazi wa Tabata Chang’ombe, wilayani Ilala.

Hata hivyo, Polisi wamesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho, huku wakisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayebainika kuhusika.

The post Polisi Wachunguza Kifo cha Mtu Aliyekutwa Bila Kichwa Mto Msimbazi – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Sbl Yashiriki Mazungumzo Ya Kuimarisha Kilimo Biashara
Next Post ‎PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 4, 2026 ‎
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook