Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Israel Yaapa Kuendeleza Mashambulizi Hadi Malengo Dhidi ya Iran Yatimizwe

  • 26
Scroll Down To Discover

Israel Defense Forces imesema iko tayari kuendelea na vita dhidi ya Iran kwa muda mrefu kadri itakavyohitajika hadi malengo ya kijeshi yatakapofikiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Reuters, msemaji wa jeshi la Israel Avichay Adraee alisema kuwa Israel itaendelea kujibu mashambulizi baada ya kundi la Hezbollah kuanzisha kile alichokiita operesheni mpya.

Jeshi la Israel pia limedai kufanya wimbi kubwa la mashambulizi katika maeneo ya Beirut nchini Lebanon jioni ya leo.

Wakati huo huo, Israel Katz, Waziri wa Ulinzi wa Israel, amesema kuwa mapigano hayo yanaweza kuendelea bila kikomo cha muda.

Amesisitiza kuwa operesheni hiyo itaendelea hadi malengo yote ya ushirikiano wa kijeshi kati ya Israel na Marekani yatakapokamilika.
Kauli hiyo inaonyesha kuwa viongozi wa Israel wanaona uwezekano wa vita hiyo kuendelea kwa muda mrefu, huku mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati ukiendelea kuongezeka.

The post Israel Yaapa Kuendeleza Mashambulizi Hadi Malengo Dhidi ya Iran Yatimizwe appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais wa Shirikisho la Soka Kongo Afungwa Jela Maisha kwa Kashfa ya Fedha
Next Post Fahamu Mambo Muhimu Yasiyotakiwa Kupuuzwa Katika Gari Lako
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook