Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Afanya Ziara ya Kikazi Bandari ya Kasanga, Aangalia Utendaji na Huduma

  • 19
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumanne (Machi 10, 2026) amekagua miundombinu na utendaji kazi wa Bandari ya Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

TPA ilifanya upanuzi wa bandari ya Kasanga mwaka 2019 kwa kuongeza urefu wa gati kutoka mita 20 hadi 120 ya kina cha mita 14 pamoja na ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na jengo la kuhudumia abiria 200 kwa wakati mmoja kwa gharama ya shilingi bilioni 4.7. Pia kumejengwa maghala mawili ya kuhifadhi mizigo yenye uwezo wa tani 2,500 kila moja.

Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Desemba 2025, bandari hiyo imehudumia jumla ya tani 3,418 za mizigo, abiria 3,648, meli 11 pamoja na maboti 337. Miongoni mwa mizigo inayohudumiwa katika bandari hiyo ni saruji, makaa ya mawe pamoja na mazao ya chakula kama mahindi, mchele na unga wa sembe.

Bandari hiyo ni miongoni mwa miundombinu ya kimkakati inayochochea shughuli za usafirishaji na biashara katika ukanda wa Ziwa Tanganyika na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Rukwa na maeneo jirani. 

RAIS TRUMP ATOA HOTUBA ya KIBABE – AJISIFIA KUIBOMOA IRAN KWA MAKOMBORA – VITA IPO PALEPALE

The post Waziri Mkuu Afanya Ziara ya Kikazi Bandari ya Kasanga, Aangalia Utendaji na Huduma appeared first on Global Publishers.



Prev Post ALAF Yatoa Viti 10 vya Magurudumu kwa Watoto Wenye Mahitaji Maalumu
Next Post Dkt. Mwigulu: Wanafunzi Bora Kusomeshwa Nje Kupitia Samia Scholarship
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook