Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Wakanusha Taarifa za Kutekwa kwa Mchungaji Yanick Mbombo

  • 31
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Mchungaji Yanick Mbombo Cele, wa kanisa la Ebenezer Restoration Ministry for all Nations, ametekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime, usiku wa Februari 22, 2026, Jeshi hilo limeeleza kushangazwa na taarifa hizo kwa kuwa mchungaji huyo, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alishafukuzwa nchini baada ya kukamilisha hukumu ya makosa mbalimbali ya jinai.

Jeshi la Polisi limebainisha kuwa Mchungaji Mbombo alikamatwa Mei 15, 2025, mkoani Iringa kwa tuhuma nzito zilizojumuisha ubakaji na mauaji ya watoto ambapo alituhumiwa kuwashawishi wafuasi wake kuwabaka watoto na kukinga damu zao kwa ajili ya maombi.

The post Polisi Wakanusha Taarifa za Kutekwa kwa Mchungaji Yanick Mbombo appeared first on Global Publishers.



Prev Post Donald Trump Ahoji Kwa nini Iran Bado Haijakubali Masharti, Atoa Siku 10 – Video
Next Post Fursa Mpya za Ajira Usichelewe! Bank Teller 13 na Supervisor 7 Wanahitajika
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook