Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Trafiki Akipigana Na Dereva, Polisi Watoa Ufafanuzi

  • 23
Scroll Down To Discover

Dodoma, Tanzania – Jeshi la Polisi nchini limezungumzia picha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikionyesha tukio la askari wa polisi (Trafiki) akizozana na dereva wa lori katika mkoa wa Dodoma.

Kupitia taarifa iliyoachiwa kwa umma, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tukio hilo halikuwa la hivi karibuni, na kwamba hatua stahiki zilichukuliwa na mamlaka husika wakati huo. Jeshi la Polisi limeongeza kuwa lilifanya ushirikiano na mamlaka nyingine kuhakikisha kuwa wahusika wanashughulikiwa kulingana na sheria za nchi.

“Jeshi la Polisi limeshughulikia kwa mujibu wa sheria kila mmoja alihusika na tukio hilo, na hatua stahiki zilichukuliwa,” ilieleza taarifa hiyo.

Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuacha kusambaza picha za matukio yaliyopita, kwani kuna hatari ya kuleta taharuki kwa jamii. Jeshi hilo pia limeongeza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu watakaoshiriki katika kusambaza picha hizo au taarifa zisizo za kweli.

The post Video: Trafiki Akipigana Na Dereva, Polisi Watoa Ufafanuzi appeared first on Global Publishers.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 22, 2026
Next Post Video: Kishandu Anusurika Kuuawa Arusha, Pikipiki Yachomwa Moto
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook