Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Radi Yaua Watu Watatu Wakivuna Mahindi, Mbeya – Video

  • 34
Scroll Down To Discover

Watu watatu wakazi wa Kitongoji cha Goye, Kijiji cha Goye, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi iliyofuatana na mvua kubwa walipokuwa wamejificha chini ya mti.

Kwa mujibu wa taarifa za familia, waliopoteza maisha ni Wilson Sanga (27), Sikuzani Tumaini Sanga (39) na Lucia Joseph Mlumbe (49).

Mashuhuda wanasema tukio hilo lilitokea majira ya saa saba mchana Februari 19, 2026, wakati marehemu walipokuwa wakivuna mahindi shambani. Mvua kubwa ilipoanza kunyesha, walikimbilia chini ya mti wa asili kujikinga, ndipo radi ilipowapiga na kusababisha vifo vyao.

Mwenyekiti wa Kitongoji alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji, ambaye aliwaarifu polisi. Askari walifika eneo la tukio na kuuchukua miili ya marehemu kisha kuipeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Makandana, Tukuyu kwa uchunguzi zaidi.

The post Radi Yaua Watu Watatu Wakivuna Mahindi, Mbeya – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Mkuu Kuanza Ziara Ya Kikazi Mkoani Arusha Februari 22, 2026
Next Post Dkt. Mwigulu Azindua Shule Mpya Ya Sekondari Ya Mbatakero
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook