Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wananchi 1,690 Walipwa Milioni 410 Kwa Madhara ya Wanyamapori Same na Mwanga

  • 38
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Wananchi 1,690 wamelipwa kifuta jasho na kifuta machozi chenye Juma ya shilingi 410,905,000 kutokana na madhara yaliyosababishwa na Wanayamapori wakali na waharibifu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wilayani Same na Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani Same Mkoani Kilimanajaro na kuongeza kuwa , Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya maboresho ya viwango vya vifuta machozi na vifuta jasho vinavyotolewa kwa wananchi wanaoathiriwa na Wanyamapori wakali na waharibifu sambamba na kuweka mfumo wa kielektroniki ili kuhakikisha waathirika wanapata kifuta jasho na kifuta machozi kwa wakati.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji

Dkt. Kijaji amewahakikishia wananchi hao, kuwa Wizara hiyo itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika kuhakikisha wanaendelea kunufaika na uhifadhi kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaongezea wananchi furaha na tabasamu kwa kuwainua kiuchumi.

Dkt. Kijaji, ameongeza kuwa, uwepo wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi na Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asiliana Chome ni chachu ya maendeleo ya wananchi hususani wa maeneo ya same kwa kuwa unatengeneza ajira na kuchangia katika pato la Taifa linalopelekea maboresho kwenye sekta mbalimbali hususani afya, Elimu na miundombinu.



Prev Post YANGA YAPANGA KUIFUTA SIMANZI YA AFRIKA
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 19, 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook