Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jeneza la Mzee Edwin Mtei Lafunikwa Bendera ya CHADEMA, Lapelekwa Tengeru – Video

  • 30
Scroll Down To Discover

Jeneza lililobeba mwili wa mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mwanzilishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mzee Edwin Mtei, leo limetolewa katika mochwari ya Hospitali ya Seliani, Jijini Arusha, likiwa limefunikwa kwa bendera ya CHADEMA.

Mwili wa marehemu umetolewa rasmi hospitalini hapo na kusafirishwa moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake Tengeru, ambako familia, viongozi wa CHADEMA pamoja na waombolezaji mbalimbali wamekusanyika kuendelea na taratibu za kumuaga.

Viongozi wa chama hicho pamoja na wananchi waliokusanyika hospitalini walionekana kuguswa na tukio hilo, wakimkumbuka Mzee Mtei kama mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika historia ya siasa za vyama vingi na sekta ya fedha nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na familia, ibada ya maziko na shughuli rasmi za kumuaga marehemu zinatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa wanatarajiwa kushiriki.

Mzee Edwin Mtei ataendelea kukumbukwa kama nguzo muhimu katika historia ya uchumi na demokrasia ya Tanzania.

The post Jeneza la Mzee Edwin Mtei Lafunikwa Bendera ya CHADEMA, Lapelekwa Tengeru – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post SIMBA ITAAMKA NA KUSONGA MBELE, CHAMA
Next Post Marekani yajiondoa rasmi W.H.O. Katika Dira ya Dunia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook