
Shirika na Project Inspire Foundation la hapa nchini kwa kushirikinana na Canada na Unicef wamezindua rasmi mradi wa vituo vya ubunifu vya Sayansi Teknolojia na uhandisi na Hisabati hapa nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi wa Inspire Foundation Project, Dk. Lwidiko Edward amesema Unicef kwa kushirikia na Project Inspire Foundation, Serikali ya Tanzania na Canada chini ya mpango unaofadhiliwa na Canada wa Every adonecent wamezindua mpango madhubuti wa kuongeza wasichana katika Sayansi Teknolojia Uhandisi na Hisabati kwa kuanzisha vituo kwenye mikoa mitatu yenye mahitaji makubwa ambayo ni Kigoma, Songwe na Tabora.
Mradi huu ambao unajulikana kama Girls Impowering STEM unatarajiwa kunufaisha wanafunzi zaidi ya 3000 na walimu zaidi ya 150 kupitia vifaa vya kidijitali, maabara za kisayansi na ushauri wa kitaaluma kutoka kwa wanawake wabobezi katika fani za sayansi, teknolojia na hisabati.
Upatikanaji wa vituo hivi vya STEM vitasaidia wanafunzi pamoja na walimu kupata uzoefu wa moja kwa moja katika nyanja ya Sayansi Teknolojia Uhandisi na Hisabati pamoja na ushauri wa kitaaluma katika ulimwengu huu karne ya 21 wa Sayansi na Teknolojia.
Mpaka sasa kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu na mwishoni mwa mwaka jana kuna hatua muhimu zimeshaanza kupatikana miongoni mwa hatua hizo ni kuungwa mkono na serikali kwenye mradi huu kwenye Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya Rais Tamisemi ambazo nazo zimeridhishwa na mradi huu na kuanzishwa vituo maalum vya STEM kwenye majengo yaliyopo mashuleni.
Pamoja na mashuleni pia vitakuwepo katika vituo vya walimu, Teachers Society na Vituo vya jamii (Community Center) ili kuongeza ushiriki wa wasichana katika STEM na kuboresha mazingira katika mazingira ya ufundishaji wa vitendo lakini pia kutumia vifaa vya kidijitali ili kuongeza usawa katika jamii.
Miongoni wa walihudhuria hafla hiyo ni Mratibu wa Mafunzo kutoka Ofisi ya Rais, Tamisemi Makao Makuu, Dodoma, Mhandisi Joyce Baravuga.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!