Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Trump Atuhumu Serikali ya Colombia Kuhusishwa na Biashara ya Dawa za Kulevya

  • 34
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani, Donald Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameibua mjadala mpana baada ya kudai kwamba huenda Jeshi la Marekani likachukua hatua za kijeshi dhidi ya Rais wa Colombia, Gustavo Petro, akidai kuwa serikali ya nchi hiyo inahusishwa na biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Trump alitoa tuhuma nzito akisema:

“Colombia inaumia. Inaongozwa na mtu ambaye, kwa maoni yangu, anahusishwa na kutengeneza na kusambaza cocaine kwenda Marekani na hilo haliwezi kuendelea kwa muda mrefu.”

Alipoulizwa iwapo anaweza kuidhinisha operesheni dhidi ya Petro kama ilivyowahi kuripotiwa kuhusu kiongozi wa Venezuela, Nicolás Maduro, Trump alisema kwamba suala hilo linaweza kuzingatiwa kwa kuwa biashara ya dawa za kulevya inaendelea kusababisha vifo vingi.

Hata hivyo, kauli hizo zimeibua wasiwasi miongoni mwa wachambuzi wa siasa za kimataifa, wakisisitiza kwamba hatua yoyote ya kijeshi inaweza kuongeza mvutano wa kidiplomasia na kuathiri usalama wa kikanda. Serikali ya Colombia haijatoa majibu ya kina kuhusu kauli hizo hadi sasa.

The post Trump Atuhumu Serikali ya Colombia Kuhusishwa na Biashara ya Dawa za Kulevya appeared first on Global Publishers.



Prev Post Nilihangaika Kwa Miaka Mitatu Kwenye Ndoa Bila Kupata Mtoto, Mbinu Hii Ikanisaidia
Next Post Dkt. Mwigulu Awasili Zanzibar Kwa Uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook